JE UKIVAA MIWANI KWA MUDA MREFU UTAKUWA TEGEMEZI KWENYE MIWANI?


 Baadhi ya watu huamini kuwa ukivaa miwani kwa muda mrefu macho yako yanaharibika na unakuwa mtu wa kutegemea miwani 👓. 

JE NI KWELI?. 

Imani hii si ya kweli.

Miwani kazi yake ni kurekebisha mwanga unao ingia kwenye jicho ili mtu aweze kuona vizuri hivyo haina uwezo wa kubadili maumbile ya jicho wala kudhuru macho. 

Hata hivyo ni vizuri kuvaa miwani yako muda wote kama ulivyoshauriwa na daktari kwani huyapumzisha macho yako na kukusaidia kutotumia nguvu nyingi kuweza kuona vizuri.

 KWANINI WATU WENGI HUAMINI KUWA MTU UKIVAA MIWANI KWA MUDA MREFU ITAKUUMIZA MACHO?? 👓

1:Mtu ambae ana tatizo la kuona vizuri kisha daktari akampatia miwani ya kumuwezesha kuona vizuri na akawa anaona vizuri atazoea hali hiyo, hivyo siku akivua miwani yake atarudi katika hali ya zamani ambayo ni kuona kwa ukungu na atahisi miwani imemuharibu, lakini si kweli bali anaona tofauti kwa sababu alizoea kuona vizuri kwa kupitia miwani. 👓

2:Kadri umri unavyo kwenda binadamu hupoteza nguvu ya macho na kupelekea mtu kushindwa kuona vitu vya karibu hasa kuanzia miaka 40 na kuendelea.Hali hii ni ya kawaida kwa kila binadamu lakini mtu kama alikuwa anatumia miwani kipindi cha nyuma na akafika umri wa kuanzia miaka 40 anahisi kama miwani imemuharibu macho kwa sababu anashindwa kuona vizuri karibu.

Imani hii si ya kweli kwani ni hali ya kawaida hata kwa ambae hakuwahi kutumia miwani. 

#SIKAFeyecare

Maoni